IQNA

Katibu Mkuu wa OIC kushiriki sherehe za utiwaji saini mapatano ya amani ya Wapalestina

13:51 - May 03, 2011
Habari ID: 2116471
Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC anatazamiwa kusafiri mjini Cairo hii leo Jumanne kwa madhumuni ya kushiriki kwenye sherehe za kutiwa saini mapatano ya umoja wa kitaifa kati ya makundi ya Palestina ya Hamas na Fat'h.
Kwa mujibu wa tovuti ya SPA mapatano hayo ambayo yameukasirisha utawala ghasibu wa Israel yatatiwa saini ya mwisho ya utekelezaji wake hii leo Jumanne huko Cairo. Katibu mkuu huyo ambaye anawakilisha nchi 57 wanachama wa OIC kwa mwaliko rasmi wa serikali ya Misri kupitia Nabil al-Arabi, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo anatazamiwa kushiriki kwenye sherehe za utiwaji saini makubaliana hayo ya mwisho ya kubuniwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina.
Tunakumbusha hapa kwamba Jumatano iliyopita makundi ya Hamas na Fat'h ya Palestina yalitangaza rasmi kufikia mapatano ya kubuniwa serikali hiyo baada ya kufanyika mazungumzo ya muda mrefu. 784936
captcha