IQNA

Msingi wa kisayansi utumike katika uchunguzi wa tarjumi za Qur'ani

21:50 - May 04, 2011
Habari ID: 2117545
Mkuu wa Taasisi ya Wahyi na Hekima yenye makao yake nchini Iran ametoa wito wa kubuniwa taasisi ya kisayansi ya kuchunguza na kutathmini tarjumi za Qur'ani Tukufu.
Katika mahojiano na IQNA, Hujjatul Islam Ali Nasiri amesema tarjumi za Qur'ani zinapaswa kuchunguzwa kwa kina kwa kutumia njia za kisayansi kabla ya kuchapishwa. Amesema, 'hili linawezekana kwa kubuni taasisi husika ya kisayansi'.
Amesema tarjumi za Qur'ani za watu binafsi si fikra nzuri tena. 'Ni bora kuwepo jopo la watarjumi na wataalamu wa sayansi za Qur'ani wanaofahamu Kiarabu na Kifarsi (au lugha nyingine) katika kazi hii'.
786095
captcha