IQNA

Malaysia kuwa mwenyeji wa maonyesho ya biashara katika ulimwengu wa Kiislamu

12:33 - May 05, 2011
Habari ID: 2117735
Kituo cha Biashara ya Kimataifa cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu kitafanya mkutano na maonyesho ya biashara na uwekezaji katika ulimwengu wa Kiislamu hapo tarehe 8 hadi 11 Juni katika mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur.
Maonyesho hayo yatafanyika kwa shabaha ya kustawisha ushirikiano wa kiuchumi na kuzidisha biashara ya ndani katika soko la kimataifa la Waislamu bilioni 1.6.
Inatazamiwa kuwa maonyesho na mkutano huo vitakuwa fursa nzuri kwa viongozi wa serikali, makampuni mbalimbali, wawekezaji wa kimataifa na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali dunia kwa ajili ya kuchunguza fursa za uwekezaji wa pamoja katika ulimwengu wa Kiislamu. 786535

captcha