IQNA

Taasisi ya Utafiti wa Nadharia za Qur’ani yaanzishwa Iran

12:16 - May 12, 2011
Habari ID: 2120852
Taasisi ya utafiti ya kustawisha nadharia za Qur’ani imeanzishwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Mafunzo ya Qur’ani nchini Iran.
Nasrallah Chamran ambaye ni msimamizi wa masuala ya logistiki katika chuo hicho amesema taasisi hiyo itafanya utafiti kuhusu sayansi za Qur’ani.
Amesema tayari watafiti wameshawasilisha makala kadhaa kuhusu maudhui mbalimbali ambazo zitashughulikuwa na taasisi hiyo. Ameongeza kuwa taasisi hiyo itakuwa na vitengo vitatua vya utafiti, elimu na sayansi.
Akielezea harakati za Chuo Kikuu cha Sayansi na Mafunzo ya Qur’ani, Chamran amesema kinatoa Shahada ya Uzamili (M.A) na Phd katika kozi 12 za vitivo vya chuo hicho.
Amesema chuo hicho kimefanikiwa kutoa mafunzo kwa wasomi wa Qur’ani ambao sasa wanajishughulisha na ustawishaji utamaduni wa Qur’ani nchini Iran.
788808


captcha