IQNA

Kikao cha pili cha kuchunguza tarjumi za Qur'ani kufanyika Tehran

12:44 - May 21, 2011
Habari ID: 2124946
Kikao cha pili kuhusu tarjumi za Qur'ani Tukufu kwa lugha nyinginezo kitafanyika leo Jumamosi Mei 21 katika makao makuu ya Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa mjini Tehran.
Chini ya anuani ya "Uchunguzi wa Tarjumi za Kiingereza za Qur'ani" kikao hicho kitahudhuriwa na Hujjatul Islam Dkt. Ahmad Ahmadi mkuu wa Taasisi ya Utafiti na Uandishi wa Vitabu vya Masomo ya Kijamii ya Vyuo Vikuu vya Iran.
Mshiriki mwingine ni Hujjatul Islam Saberi Mkurugenzi wa Kituo cha Kuratibu Uchapishaji naTarjumi za Vitabu ya Kiislamu.
Kikao hicho kimeandaliwa na IQNA, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sayansi na Mafunzo ya Qur'ani.
Kikao cha kwanza katika mfululizo wa vikao hivyo vya kuchunguza tarjumi za Qur'ani kilifanyika Mei 3 na kuhudhuriwa na Dkt. Salar Manafai Anari na Dkt. Hussein Mollanazar.
793988
captcha