OIC imetoa wito kwa serikali ya Misri kufungua kivuko cha Rafah ambacho hutumiwa na wakazi wa Ghaza kuingiza bidhaa muhimu.
Katika ripoti yake kuhusu hali ya kibinadamu ya Ukanda wa Ghaza, OIC imesema kuwa asilimia 98 ya viwanda vya Ghaza vimefungwa tokea uanze mzingiro wa eneo hilo jambo ambalo limepelekea kuzorota zaidi hali ya kiuchumi, kimaisha na kijamii ya wakazi wa Ghaza.
Ripoti hiyo ya OIC imeongeza kuwa katika vita vya siku 22 vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza vilivyoanza mwezi Desemba 28 mwaka 2008, sekta binafsi Ghaza ilipata hasara ya zaidi ya dola milioni 400.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekaidi matakwa ya jamii ya kimataifa ya kuutaka usitishe mzingiro wake wa kinyama dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Mzingiro huo wa Wazayuni ulianza mwaka 2007 baada ya Wapalestina kuichagua kwa njia ya demokrasia Harakati ya Mapambano ya Kiislamu, Hamas, kuongoza Ghaza. Wapalestina zaidi ya milioni moja na nusu wako chini ya mzingiro wa kinyama wa Wazayuni ambapo wananyimwa uwezo wa kupata mahitajio ya kila siku kama vile chakula, dawa na nishati.
796000