Kituo cha habari cha el Watan kimeripoti kuwa kongamano hilo litahudhuriwa na wataalamu wa sheria, washauri wa masuala ya familia, maulamaa wakubwa wa Algeria na wahadhiri wa vyuo vikuu katika Chuo Kikuu cha Amir Abdul Qadir.
Miongoni mwa maudhui zitakazojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na ‘aya za Qur’ani na hadithi zinazohusiana na watoto’, ‘embriolojia au taaluma ya maisha ya kiinitete katika aya za Qur’ani’, ‘watoto na haki zao za kupata elimu kwa mujibu wa suna na hadithi za Mtume (saw)’ na ‘uhusiano wa baba na watoto katika sheria za Kiislamu’.
Sehemu nyingine ya kongamano hilo itashughulikia makala za wasomi na wataalamu wa masuala ya kidini kuhusu haki za watoto Waislamu katika jamii zisizokuwa za Kiislamu.
Vi vyema kukumbusha hapa kuwa nchi nyingi duniani huadhimisha tarehe Mosi Juni kama Siku ya Kimataifa ya Watoto. 797444