IQNA

Washindi wa kike wa Mashindano ya Qur'ani Gambia wapewa zawadi

17:47 - May 25, 2011
Habari ID: 2128587
Washindi wa kike wa mashindano ya Qur'ani Gambia wamekabidhiwa zawadi katika sherehe zilizofanyika katika Ikulu ya Rais katika mji mkuu wa nchi hiyo Banjul.
Sherehe hizo za Ijumaa iliyopita zilihudhuriwa na Rais Yahya Jame ambaye katika hotuba yake alisisitiza kuwa Uislamu ni dini ya amani.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Kiislamu IINA, mshindi wa kike katika Mashindano ya Qur'ani ya walio chini ya umri wa miaka 19 yaliyodhamniniwa na Rais wa Gambia alikuwa Bi Zeinab Mohammad Cham huku Maryam Yahya akichukua nafasi ya pili na Hassanatou Abdourahman akichukua nafasi ya tatu.
Mashindano ya Qur'ani nchini Gambia yametajwa kuwa chombo cha kutangaza Uislamu nchini humo na kutoa fursa kwa vijana Waislamu kuonyesha umahiri wao.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Elimu, Utafiti, Sayansi na Teknolojia nchini Gambia Dr. Mariam Sarr Ceesay amesema wanawake wana nafasi muhimu katika dini ya Kiislamu. Amesema Waislamu wanapaswa kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kufuata sira ya Mtume SAW.798343
captcha