IQNA

Ujenzi wa vitongoji vya Wazayuni ni hatari kwa Msikiti wa Al Aqsa

22:29 - May 25, 2011
Habari ID: 2128636
Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Msikiti wa Al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni hatari kwa msikiti huo ambao ni sehemu ya tatu takatifu zaidi kwa Waislamu duniani.
Jumatano iliyopita mawaziri wa utawala wa Kizayuni wa Israel walisherehekea ufunguzi wa nyumba 1,000 za walowezi wa Kiyahudi katika mtaa wa Kipalestina wa Ras al Amud katika eneo la Mlima wa Zeitun mjini Quds.
Taasisi ya Waqfu na Turathi ya Al Aqsa imetoa taarifa na kusema utawala wa Kizayuni unapanga kujenga nyumba zaidi za walowezi wa Kiyahudi katika eneo hilo. Taarifa hiyo imesema kitongoji kipya kinachopanga kujengwa hapo kutakuwa na daraja itakayounganishwa na Msikiti wa Al Aqsa.
Taasisi ya Waqfu na Turathi ya Al Aqsa imeonya kuwa utawala wa Kizayuni umetoa wito kwa Mayahudi kuhamia katika kitongoji hicho kwa sababu kiko karibu na Al Aqsa.
Viongozi wa Palestina wametoa wito kwa nchi za Kiislamu duniani kuchukua hatua za kivitendo kukabiliana na njama za Wazayuni za kuharibu Msikiti wa Al Aqsa ambao ndio kibla cha kwanza cha Waislamu.
798401
captcha