IQNA

Kituo cha Utamaduni cha Ahul Bayt AS chafunguliwa Berlin

10:58 - May 30, 2011
Habari ID: 2130474
Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ujerumani imetangaza kuwa Kituo cha Utamaduni cha Ahlul Bayt AS kimefunguliwa mjini Berlin.
Kituo hicho kimefunguliwa Mei 24 sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra AS. Sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa na viongozi wa kidini na kiutamaduni wa Ujerumani na maeneo mengine ya Ulaya.
Kituo hicho kiko chini ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS na kinatazamiwa kuendesha shughuli zake chini ya usimamizi wa Ayatullahil Udhma Ali Sistani.
Wakati huo huo Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Ujerumani imetoa toleo la 92 la Jarida la Kila Wiki la Utamaduni. Jarida hilo huakisi habari za Kiislamu nchini Ujerumani na maeneo mengine ya Ulaya.
800070
captcha