Sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na Salman bin Abdul Aziz, Amir wa eneo la Riyadh, zitaenzi na kuwapa zawadi washindi wa kike na kiume 28 walioshinda mashindano hayo ya kitaifa ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudia tokea tarehe 9 hadi 15 za mwezi huu wa Mei ambapo wavulana 15 na wasichana 13 walitangazwa kuwa washindi wa mwisho.
Mashindano hayo yalifanyika katika hatua tano za hifdhi ya Qur'ani nzima sambamba na usomaji wa tartili, tajwidi na tafsiri ya maneno ya Qur'ani, hifdhi ya Qur'ani nzima, usomaji na tajwidi, hifdhi ya juzuu 20 sambamba na usomaji na tajwidi, hifdhi ya juzuu 10 zinazofuatana inayoandamana na usomaji pamoja na tajwidi na hifdhi ya juzuu 5 zinazofuatana pamoja na usomaji na tajwidi. 801508