Kwa mujibu wa tovuti ya Zawya benki hiyo ya Kiislamu imeahidi kushirikiana na shirika hilo la Msalaba Mwekundu kwa madhumuni ya kuimarisha thamani na malengo ya kiutu pamoja na kukidhi mahitaji ya kijamii.
Kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa, benki hiyo itakuwa ikidhamini gharama za masomo kwa wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia karo za shule na wale walio na hamu ya kunufaika na masomo yanayotolewa katika vituo maalumu vya masomo ya kitaalamu. 802694