Hujjatul-Islam Sidiqi amekumbusha kuwa mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 yaliyoongozwa na Imam Khomeini (M.A) hapa nchini Iran yalikuwa na lengo la kumkomboa kila mpenda haki duniani. Akifafanua zaidi shaksia ya Imam Khomeini (M.A), Hujjatul-Islam Hassan Sidiqi amesema kuwa muasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliweza kuchora msitari wa kupambanua kati ya mabeberu na wapenda haki. Amesema Waislamu wanayo mengi ya kujifunza kutokana na harakati za ukombozi za Imam Ruhullah Khomeini.
803199