IQNA

Kongamano la Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa katika Hija kufanyika Saudia

15:56 - June 06, 2011
Habari ID: 2133789
Kongamano la Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa katika Hija limepanwa kuanyika tarehe 12 hadi 17 Juni katika Chuo Kikuu cha Ummul Quraa mjini Makka.
Kongamano hilo linafanyika kwa lengo la kuchunguza teknolojia ya kisasa na njia za kuitumia katika kuboresha safari za hija.
Jumuiya mbalimbali zinazohusika na masuala ya hija, viongozi wa kidini wa Saudia na mashirika yanayotoa huduma za masuala ya ziara na hija yatatoa mapendekezo yao kuhusu jinsi ya kusimamia ibada ya hija kwa njia bora zaidi.
Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na takwimu za mahujaji wanaozuru Msikiti wa Mtume (saw) mjini Madina, mipango ya kuzidisha mabustani ya umma katika miji ya Makka na Madina, mbinu za kusafirisha mahujaji, uboreshaji wa usafiri wa umma na masuala ya afya ya mahujaji. 803943
captcha