IQNA

Kongamano la ‘Nafasi ya Wanawake Waislamu katika Mwamko wa Kiislamu’

14:13 - June 11, 2011
Habari ID: 2135606
Kongamano la ‘Nafasi ya Mwanamke katika Mwamko wa Kiislamu’ limefanyika Juni 9 katika mji wa Zanjan, kaskazini magharibi mwa Iran.
Kongamano hilo lilifunguliwa kwa hotuba ya Imamu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Khodabandeh Hujjatul Islam Ali Tahmasebi.
Aliashiria njama za maadui dhidi ya nchi za Kiislamu na kusema, ‘mwamko wa Kiislamu umewatia wasiwasi maadui wa Uislamu na sasa wanajaribu kuzuia kuenea dini tukufu ya Kiislamu kwa kueneza ufisadi na ufuska miongoni mwa Waislamu hasa wanawake’.
Amesisitiza umuhimu wa vazi la hijab na kulinda heshima miongoni mwa wanawake Waislamu. Amesema kujiheshimiwa vazi la hijabu ya wanawake Waislamu ni mambo ambayo yanayatia wasiwasi madola ya kibeberu duniani.
Mwanazuoni huyo amesema wanawake Waislamu wa Iran kwa kuendeleza harakati zao za kijamii kwa kuzingatia maadili ya Kiislamu wamekuwa kigezo cha kuigwa na wanawake wote duniani.
Kwingineko katika hotuba yake, Imamu wa Sala ya Ijumaa mjini Khodabandeh amelaani mauaji ya watoto na wanawake Waislamu nchini Bahrain. Amesema ukatili huo wa utwala wa Aal Khalifa unaoungwa mkono na Marekani unatokana na kuwa wanawake wa Bahrain wanafuata mafundisho halisi ya Uislamu.
805797

captcha