IQNA

Shirika la Awqaf Iran huandaa mashindano 1,600 ya Qur'ani kila mwaka

14:59 - June 13, 2011
Habari ID: 2137477
Shirika la Awqaf na Misaada la Iran huandaa mashindano zaidi ya 1,600 ya Qur'ani kila mwaka nchini Iran katika viwango mbalimbali.
Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika Shirika la Awqaf Hujjatul Islam Ahmad Sharafkhani alikuwa akizungumza Juni 12 katika mkutano na waandishi habari kuhusu mikakati ya shirika hilo katika msimu wa joto.
Amesema mashindano hayo hufanyika katika miji, mikoa na kitaifa katika viwango mbalimbali kama vile qiraa, hifdhi na vilevile adhana.
Amesema kila mwaka katika miji 280 kote Iran hufanyika mashindano ya Qur'ani yaliyoandaliwa na shirika la Awqaf.
Ameongeza kuwa kwa wastani kila shindano la Qur'ani huwa na majaji watano. Amesema mashindano ya Qur'ani katika miji kwa msimu wa joto mwaka huu yameanza na yataendelea hadi Septemba mosi.
807217
captcha