Kituo cha Palestine Info kimerpoti kuwa, katika ripoti hiyo UNICEF imetangaza kwamba askari wa utawala ghasibu wa Israel wameua watoto 10 wa Kipalestina na kujeruhi wengine 117 katika kipindi cha miezi ya Machi na Aprili.
Ripoti hiyo mesisitiza kuwa mashambulizi ya askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watoto wadogo wa Palestina yameongezeka maradufu katika miezi hiyo miwili.
Imesema kuwa asilimia 44 ya mauaji hayo yamefanyika katika Quds Tukufu.
Shirika la UNICEF limeitaka jamii ya kimataifa kufanya uchunguzi kuhusu mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya watoto wa Palestina na kuwafikisha mahakamani wahusika. 807967