IQNA

Nakala za maandishi ya mkono ya Bosnia kuonyeshwa Kuwait

13:55 - June 23, 2011
Habari ID: 2143133
Kuwait imekuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu mwenyeji wa maonyesho ya nakala za maandishi ya mkono na vitabu vya Kiislamu kutoka Bosnia Herzegovina.
Shirika la habari la Kuwait KUNA limeripoti kuwa maonyesho hayo yanayosimamiwa na Baraza la Taifa la Utamaduni la Kuwait (NCCAL) yanajumuisha vitabu 366 na nakala 700 za maandishi ya mkono yaliyokusanywa na Dakta Safvet beg Basagic.
Safvet beg Basagic (1870-1934) maarufu kwa jina la Mirza Safvet alikuwa mwandishi wa Kibosnia na baba wa mageuzi ya nchi hiyo. Vilevile alikuwa malenga mashuhuri mwanzoni mwa karne ya 20. Safvet beg Basagic pia ndiye mwasisi wa Jumuiya ya Utamaduni ya Gojrat na alikuwa kiongozi wa Baraza la Bosnia katika mwaka 1910.
Katika kipindi cha uhai wake mwandishi huyo alikusanya majmui ya nakala nadra na zenye thamani kubwa za Kiislamu na vitabu vya kale vinavyohifadhiwa katika maktaba ya Chuo Kikuu cha mji mkuu wa Slovakia, Bratislava. 813533

captcha