Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Sayyid Ali Akbar Husseini mkuu wa kitengo cha tarjumi na tafsiri katika Taasisi ya Utamaduni na Mafunzo ya Qur’ani.
Kituo hicho kitakuwa na jukumu la kuwakusanya pamoja wataalamu wa tarjumi ya Qur’ani nchini na kuwasilisha maelezo ya kiufundi.
Amesema taasisi hiyo tayari inajishughulisha na kazi za tarjumi na tafsiri. Ameongeza kuwa utafiti unafanyika kuhusu mahitajio ya wanafunzi katika viwango mbalimbali.
816816