‘Ni matumaini yangu kuwa Waislamu watatambua umuhimu wa tukio hili ili kuwa na umoja. Tabia bora ya Muislamu itaimarisha moyo wa umoja na amani katika taifa’, amesema.
Katika salamu zake kwa mnasaba wa kumbukumbu ya tukio la Israa na Mi’raj, Waziri Mkuu wa Malaysia ametoa wito kwa Waislamu kupata ibra katika safari ya Mtume Muhammad SAW katika tukio la Isra na Mi’raj. Ameongeza kuwa kupata funzo kuhusu tukio hilo kutaliongoza taifa la Malaysia katika kufikia malengo ya ustawi ya mwaka 2020.
Waziri Mkuu wa Malaysia amesema kwa kuzingatia uhusiano wa karibu wa tukio la Israa na Mi’iraj na Msikiti wa Al Aqsa ambao ulikuwa kibla cha kwanza cha Waislamu, kuna haja ya Waislamu kupambana kwa ajili ya kuwakomboa Wapalestina kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Ameongeza kuwa funzo jingine la tukio la Israa na Mi’raj ni amri ya Allah kuhusu sala tano za kila siku kwa Waislamu.
817511