IQNA

Iran kuzindua mpango maalumu wa kuhifadhi Qur’ani

8:08 - July 04, 2011
Habari ID: 2148314
Mpango maalumu kuhusu kuhifadhi Qur’ani Tukufu utaanzishwa katika vyuo vikuu vya sayansi za Qur’ani kote nchini Iran.
Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Alireza Shasavani amesema kozi hiyo itawahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu vya sayansi za Qur’ani na mafundisho ya Kiislamu.
Amesema wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza watahifadhi juzuu kadhaa katika msimu wa majira ya joto na hatimaye katika kipindi chote cha mwaka wanatazamiwa kuhifadhi Qur’ani nzima.
Amesema washiriki watahifadhi kurasa mbili za Qur’ani kila siku na watahudhuria darsa za tafsiri kabla ya kuhifadhi.
818439
captcha