IQNA

Kustawisha tafakuri ya Qur’ani ni moja ya malengo ya mashindano ya Qur’ani

8:19 - July 04, 2011
Habari ID: 2148316
Mkuu wa masuala ya utamaduni katika Shirika la Awqaf la Iran amesema kuhimiza mwenendo wa kutafakari aya za Qur’ani ni moja ya malengo ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Tehran.
Akizungumza katika kongamano la ‘Utafiti wa Qur’ani’ mjini Tehran, Hujjatul Islam Ahmad Sharafkhani amesema kuwa kwa kuzingatia hilo, Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani yalianzisha kitengo cha kuandika makala miaka minne iliyopita.
Ameongeza kuwa katika kitengo cha makala mwaka huu, mada nne ambazo zinajadiliwa ni ‘Mwamko wa Kiislamu kwa mtazamo wa Qur’ani’, ‘Kuifahamu Qur’ani’, ‘Bidii katika Mtazamo wa Qur’ani’ na ‘Kutambua Fitina kwa Mtazamo wa Qur’ani’. Makala 521 ziliwasilishwa ambapo 15 ziliteuliwa kwa ajili ya mashindano.
Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran yalianza tarehe 27 Rajab na yanatazamiwa kumalizika tarehe Pili Shaaban.
819206
captcha