Qasim Shuaib Abubakar ambaye anawakilisha Ghana katika Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu amesema: ‘Nahisi furaha kubwa kushiriki katika hafla hii kubwa. Ni fursa kwangu kuanzisha mawasiliano na makarii na mahufadh kutoka maeneo yote ya dunia’,
Amepongeza waandalizi na kuwahimiza kuongeza idadi ya nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo.
Abubakr amewashukuru maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa juhudi zao za kustawisha harakati za Qur’ani. Ameongeza kuwa: 'Ziara yangu katika Haram ya Imam Khomeini RA ilikuwa muhimu sana na imenisaidia kuifahamu Iran.'
Abubakr mwenye umri wa miaka 27 ni mwanafunzi wa chuo kikuu na anasema kuhifadhi Qur’ani kumekuwa na taathira nzuri katika maisha yake.
818623