Rahmati Muhamamd ambaye amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Misri nchini Indonesia amekitaka Chuo Kikuu cha al Azhar kuunga mkono suala la kuanzishwa Kituo cha Mazungumzo kati ya Tamaduni Mbalimbali katika mji huo.
Lengo la kuasisiwa kituo hicho limetajwa kuwa ni kuweka wazi sura halisi ya Uislamu wenye misimamo ya wastani na kukifanya kituo cha mazungumzo katika eneo la Asia na Pacific.
Kwa upande wake balozi wa Misri mjini Jakarta amesema al Azhar imeanza harakati za kuanzisha mazungumzo kati ya wafuasi wa dini na tamaduni tofauti duniani. Ameongeza kuwa atawasilisha ombi hilo kwa Sheikh wa al Azhar Ahmad al Tayyib. 825258