IQNA

Tamasha ya watoto kuhusu mwamako wa Imam Hussein AS yapangwa Karbala

9:17 - July 14, 2011
Habari ID: 2154240
Tamasha ya Kimataifa ya Watoto Kuhusu Mwamko wa Imam Hussein AS imepangwa kufanyika Karbala nchini Iraq.
Kwa mujibu wa tovuti ya Noon, tamasha hiyo imeandaliwa na Idara ya Watoto katika Haram ya Imam Hussein AS. Tamasha hiyo itawakutanisha watoto waliochini ya umri wa miaka 12 kutoka nchi kadhaa duniani.
Ali Kazem Soltan ambaye ni mkuu wa masuala ya habari katika Haram ya Imam Hussein AS amesema lengo la tamasha hiyo ni kujaribu kuwaeleza washiriki kuhusu mwamko wa Imam Hussein AS na tukio la Ashura.
Tamasha hiyo itajumuisha mijadala, mashairi, uchoraji, kaligrafia na makala.
823994
captcha