Muhammad Abumalha amesema kuwa matayarisho ya mashindano hayo yatakayofanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani yamekamilika.
Ameongeza kuwa Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tuzo ya Dubai imewasiliana na Wizara za Wakfu na Masuala ya Kiislamu katika nchi za Kiislamu na vituo rasmi vya Kiislamu katika jamii zisizokuwa za Waislamu na kuwaalika katika mashindano hayo.
Abumalha ambaye pia ni mshauri wa masuala ya kiutamaduni wa Gavana wa Dubai amesema mashindano ya mwaka huu ya Qur'ani ya Dubai yatawashirikisha watu kutoka nchi mbalimbali na kwamba baadhi ya nchi hizo zitashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo kama Ireland. Amesema kuwa mshiriki kutoka nchi hiyo ni mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 8 ambaye amehifadhi Qur'ani nzima. 828501