Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Sala ya Ijumaa katika uwanja wa Chuo Kikuu chaTehran na kubainisha kwamba, matakwa ya wananchi wa Misri ni kushtakiwa viongozi waliotenda jinai katika kipindi cha utawala wa dikteta Hosni Mubarak.
Ayatullah Khatami ameashiria ujumbe wa Marekani kwa serikali ya mpito ya Misri wa kuikatia misaada nchi hiyo endapo itachukua misimamo iliyo dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema kwamba, Washington imeingiwa na kiwewe na wasi wasi mkubwa wa kuwa hatarini maslahi ya Israel huko Misri.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuhusiana na matukio ya Bahrain kwamba, muqawama na kusimama kidete wananchi wa nchi hiyo katika kukabiliana na kupenda makuu kwa utawala wa kifalme wa Aal-Khalifa ni jambo linalopaswa kusifiwa.
829401