IQNA

Mshindano ya Qur’ani ya Kimataifa ya Malaysia kumalizika leo

10:46 - July 23, 2011
Habari ID: 2158147
Mashindano ya 53 ya Qur’ani ya Kimataifa ya Malaysia yanamalizika leo katika Kituo cha Kimataifa cha Putra mjini Kuala Lumpur.
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo Hamid Shakirnejad ameliambia shirika la habari la IQNA kwamba sherehe za kufunga mashindano hayo ya Qur’ani zitafanyika jioni ya leo kwa wakati wa Malaysia.
Amesema Mashindano ya 53 ya Qur’ani ya Kimataifa ya Malaysia yamefanyika katika vitengo viwili vya wanawake na wanaume na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa kila kitengo watatangazwa leo na kutunukiwa zawadi zao.
Kuhusu programu na shughuli nyingine zinazofanyika katika mashindano hayo, karii huyo wa kimataifa wa Iran amesema mashindano ya Qur’ani ya Malaysia hayakuwa na kiraa ya pambizoni mwa mashindano rasmi kama ilivyofanyika katika mashindno ya Qur’ani ya Tehran na kwamba washiriki katika mashindano hayo walikuwa wakitumbuizwa kwa kasida.
Akifanya ulinganisho baina ya Mashindano ya Qur’ani ya Kimataifa ya Iran na yale ya Malaysia, Shakirnejad amesema mashindano hayo mawili yamefanyika katika viwango sawa japokuwa mashindano ya Qur’ani ya Iran yafanyika katika vitengo vingi zaidi kama kiraa na hifdhi ilhali yale ya Malaysia yanafanyika katika kiraa peke yake. 829676

captcha