Dakta Larijani ameitaka Marekani kufikiri upya misimamo yake dhidi ya Iran na kuelewa kwamba matendo yake hayo ya kigaidi yatakuwa na athari mbaya katika siku za usoni.
Spika wa Bunge la Iran aidha amevitaka vyombo vya usalama vya hapa nchini kuwa macho zaidi ili kuweza kukabiliana na njama za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Adhuhuri ya jana magaidi walimpiga risasi na kumuua Dariush Rezaeinejad, mhadhiri wa moja ya vyuo vikuu hapa nchini Iran. Huko nyuma pia magaidi ambao walibainika kuwa vibaraka wa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi na utawala wa Kizayuni, waliwaua wataalamu wa nyuklia hapa nchini. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kupiga hatua kubwa katika uga wa nyuklia kwa kutegemea wataalamu wa hapa nchini.
Duru za polisi mjini Tehran zimedokeza kuwa Daryoush Rezaeinejad aliyekuwa na umri wa miaka 35 aliuawa kigaidi Jumamosi karibu na nyumbani kwake mjini Tehran.