IQNA

Msikiti wa Strasbourg, mwenyeji wa vikao vya Qur'ani mwezi Ramadhani

9:22 - July 25, 2011
Habari ID: 2159313
Vikao vya kiraa ya Qur'ani Tukufu vitafanyika katika msikiti mpya wa Strasbourg nchini Ufaransa.
Msikiti huo ambao utafunguliwa sambamba na kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, unataka kuanza kazi zake kwa nuru ya vikao vya kiraa ya Qur'ani Tukufu.
Viongozi wa Msikiti wa Stasbourg wametangaza kuwa vikao vya kiraa ya Qur'ani Tukufu vitawashirikisha wasomaji mashuhuri wa Qur'ani na kwamba kutakuwepo mihadhara itakayojadili masuala mbalimbali ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Msikiti mkubwa wa Strasbourg utafunguliwa kwa ajili ya Waislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ruhusa ya meya wa mji huo na kisha utafungwa kwa kipindi cha miezi miwili kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake. 830365
captcha