IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika Burundi

9:20 - July 25, 2011
Habari ID: 2159314
Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu ya wanafunzi wa vyuo vikuu yalifanyika juzi katika Msikiti wa Tauhidi katika eneo la Buyenzi mjini Bujumbura yakiwashirikisha wanawake na wanaume.
Mashindano hayo yamesimamiwa na ofisi ya Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu (MWL) nchini Burundi na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani yakiwashirikisha wanafunzi 53 wa vyuo vikuu.
Mashindano hayo yamefanyika katika vitengo vitatu vya hifdhi ya Qur'ani nzima, hifdhi ya juzuu 15 na hifdhi ya juzuu 7.
Sherehe za kuwatunza washindi katika mashindano hayo ya Qur'ani zilihudhuriwa na Mufti wa Burundi Sheikh Shaaban Umar, viongozi na wawakilishi wa jumuiya na taasisi za Kiislamu. 830547

captcha