Mkuu wa kamati andalizi ya mashindnao hayo Farhan al Ka'abi amesema mashindano hayo yatakuwa katika kitengo cha hifdhi na yatamalizika tarehe 20 mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Amesema washindi watatunukiwa zawadi katika sherehe za kufunga mashindano.
Amesema pembizoni mwa mashindano hayo kutakuwa na shughuli kadhaa kama vile: 'Ramadhani Inahitaji Watu Wapya'. Mpango huo unalenga kuiarifisha dini tukufu ya Kiislamu kwa wasiokuwa Waislamu.
Aidha kutakuwa na mpango wa kuwaenzi wanafunzi na mahufadh wa Qur'ani katika vyuo mbalimbali vya Imarati katika fremu ya kauli mbiu ya "Qur'ani inaposomwa, Umma wa Kiislamu Unastawi".
831061