IQNA

Tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Fulani yazinduliwa Nigeria

12:39 - July 26, 2011
Habari ID: 2160216
Tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Fulani imezinduliwa katika mji wa Yola katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria katika sherehe iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais wa nchi hiyo.
Akizungumza katika halfa hiyo ya kuzinduliwa tarjumi ya Qur'ani ya Kifulani Makamu wa Rais wa Nigeria Namadi Sambo amesema mzozo katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo unaweza kuzuiwa iwapo watu wataifahamu Qur'ani ipasavyo. Ametoa wito kwa Waislamu kuzingatia mafundisho ya Kiislamu kwani hiyo ndio njia bora zaidi ya watu kuishi pamoja kwa usalama na kustawisha nchi.
Makamu wa Rais wa Nigeria amewapongeza wale waliochukua hatua ya busara ya kuitarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kifulani.
Akizungumza katika hafla hiyo Sultan wa Sokoto Al Haji Sa'ad Abubakar III amesema tukio hilo ni muhimu na la kihistoria katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesema mbali na nchini Nigeria, lugha ya Kifulani inazugumzwa na watu wengi Cameroon, Chad na Mali.
831800
captcha