Mwandishi wa Misri Sayyid al Qamni alitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2009 kupitia Baraza Kuu la Utamaduni la serikali ya dikteta aliyeng'olewa madarakani. Kamati Kuu ya Baraza la Serikali ya Misri imemnyang'anya tuzo hiyo na kusema kuwa mitazamo iliyomfanya mwandishi huyo apewe tuzo hiyo maalumu ya serikali inapingana na Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume Muhammad (saw).
Katika vitabu vyake, mwandishi huyo ametilia shaka hata asili na nasaba za baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuwafanyia maskhara wajumbe hao wa Allah. Si hayo tu bali alidhubutu hata kuivunjia heshima dhati tukufu ya Mwenyezi Mungu (sw).
Baada ya kuondolewa madarakani serikali ya kidikteta ya Hosni Mubarak mawakili kadhaa wa Misri waliwasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya mwandishi huyo na kutaka anyang'anywe tuzo ya serikali ya mtaalamu bora wa masuala ya jamii na kufikishwa mahakamani waliompa tuzo hiyo.
Wanasheria hao wamesema wanaamini uhuru wa itikadi na fikra lakini suala hilo si sababu ya kuvunjiwa heshima matukufu na thamani za kidini na kijamii za wananchi.
831813