IQNA

Mkutano wa Kimataifa wa Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali kufanyika Ujerumani

13:56 - July 26, 2011
Habari ID: 2160337
Mkutano wa Kimataifa wa Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali utafanyika tarehe 11 hadi 14 Septemba katika mji wa Munich nchini Ujerumani. Mkutano huo utasimamiwa na Kanisa la Munich likishirikiana na taasisi nyingine ya kidini.
Mkutano huo ambao utafanyika kwa kaulimbiu ya 'Jisabilie kwa Ajili ya Kuishi na Wenzako' utahudhuriwa na wawakilishi wa dini za Kiislamu, Kikristo na Kiyahudi kutoka nchi 60 duniani.
Mkutano huo utafunguliwa na Rais Christian Wulff wa Ujerumani na katika siku ya pili utahutubiwa na Kansela Angela Merkel wa nchi hiyo ambaye atazungumzia mchango wa mazungumzo kati ya dini mbalimbali katika kuboresha hali ya kijamii na kiutamaduni ya raia.
Miongoni mwa shakhsia wa Kiislamu watakaoshiriki katika mkutano huo ni msemaji wa Chuo Kikuu cha al Azhar cha Misri Muhammad Rafa'a Tahtawi, Mwenyekiti wa Kituo cha Kiislamu cha New Delhi Wahhabuddin Khan na Said Aqiil Siraj ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nah'dhatul Ulamaa ya Indonesia.
Vilevile inatazamiwa kuwa wawakilishi wa dini kama za Budha na Hindu watashiriki katika mkutano huo. 831706


captcha