IQNA

Nchi 50 kushiriki Mashindano ya Qur'ani ya Kimataifa ya Algeria

14:36 - July 27, 2011
Habari ID: 2160984
Naibu Waziri wa Wakfu ya Masuala ya Kidini wa Algeria Edah Falahi amesema nchi 50 za Kiislamu zimetangaza kuwa ziko tayari kushiriki katika Mashindano ya 8 ya Qur'ani ya Kimataifa yatakayofanyika nchini humo.
Edah Falahi amesema kuwa nchi hizo 50 zimetangaza kuwa ziko tayari kushiriki katika Mashindano ya 8 ya Qur'ani ya Kimataifa yatakayofanyika mwezi Ramadhani katika mji wa Tlemcen huko magharibi wa Algeria. Ameongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa mnasaba wa kutangazwa mji wa Tlemcen kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2011.
Amesema kuwa mbali na nchi za Kiislamu, wawakilishi wa baadhi ya nchi zisizokuwa wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kama Hungary na Korea Kusini watashiriki katika mashindano hayo. Amesema kushirikishwa nchi zisizokuwa za Kiislamu katika mashindano hayo kunafanyika kwa lengo la kuwahamasisha Waislamu wanaoshi katika nchi hizo ili washiriki katika shughuli za kimataifa za Kiislamu na kuimarisha moyo wa uvumilivu na kuishi pamoja kwa amani.
Naibu Waziri wa Wakfu wa Algeria amesema pambizoni mwa mashindano hayo ya Qur'ani ya kimataifa kutafanyika mashindano ya hifdhi ya Qur'ani kwa ajili ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 15. 832454



captcha