Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiye atakayefungua rasmi maonyesho hayo katika sherehe ambazo zitawashirikia maelfu kadhaa ya wapenzi wa Qur'ani Tukufu.
Maonyesho ya mwaka huu ya Qur'ani Tukufu yatajumuisha vitengo 30 vikiwemo vya watoto wadogo, mabarobaro, picha, familia, mwamko wa Kiislamu, sanaa mbalimbali za picha na tamthilia, bidhaa za kiutamaduni, mapinduzi ya kisayansi ya mwanaadamu, staha na Hijabu pamoja na masuala ya fasihi na mashairi.
Ukiachilia mbali masuala ya vitabu vinavyohusiana na Qur'ani Tukufu, ratiba nyingine zitakazokuwemo kwenye maonyesho hayo ni pamoja na vikao vya kitaalamu, programu mbalimbali za kompyuta kuhusu Qur'ani Tukufu, athari za kisanii n.k.
Mbali na Iran, nchi nyingine 30 zinatarajiwa kushikiri kwenye Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ambayo hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho hayo yanatazamiwa kuendelea hadi tarehe 26 Agosti katika eneo la Uwanja Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini hapa Tehran.
832823