Rais Ahmadinejad aliyasema hayo jana jioni katika ufunguzi wa maonyesho ya 19 ya Qur'ani Tukufu ya Kimataifa mjini Tehran. Ameongeza kuwa Qur'ani Tukufu ni kitabu cha dunia nzima, mwongozo wa mwanadamu na njia ya kumfikisha kiumbe huyo kwenye kilele cha ukamilifu. Amesema kuwa adhama na utukufu wa Mwenyezi Mungu (sw) unaonekama kikamilifu katika kitabu cha Qur'ani Tukufu.
Rais Amadijenad pia ameashiria kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani na uhusiano wa mwezi huo na Qur'ani na akasema njia ya uokovu wa mwanadamu imo katika kushikamana na Qur'ani.
Maonyesho ya 19 ya Qur'ani ya Kimataifa yaliyoanza jana yataendelea hadi taheye 26 Agosti sawa na tarehe 26 Ramadhani. 833295