IQNA

Kongamano la kwanza la kitaifa la Qur’ani laanza Nasiriyya, Iraq

23:50 - July 30, 2011
Habari ID: 2162240
Kongamano la kwanza la kitaifa la Qur’ani Tukufu limeanza leo Jumamosi katika mji wa Nasiriyya mkoani Dhiqar nchini Iraq chini ya usimamizi wa Kamati Kuu ya Kudumu ya Qur’ani Tukufu ya Baraza la Mawaziri la Iraq.
Mkurugenzi wa taasisi ya Darul Qur’ani ya mji wa Nasiriyya Raad Adnan ameliambia shirika la habari la IQNA kwamba kongamano hilo limenza leo asubuhi na kwamba linahudhuriwa na wapenzi wa Qur’ani kutoka mikoa ya Baghdad, Misan al Muthanna, Najaf na Karbala.
Amesema kongamano hilo linajadili sababu za umma wa Kiislamu kuwa mbali na Qur’ani na njia za kuondoa tatizo hilo. Amesema maudhui nyingine inayojadiliwa ni fasaha na balagha ya Qur’ani Tukufu.
Raad Adnan ameongeza kuwa miongoni mwa ajenda za kongamano hilo ni vikao vya kiraa ya Qur’ani Tukufu itakayowashirikisha makarii mashuhuri wa mikoa inayoshiriki katika kongamano hilo. 833708
captcha