Shirika la habari la Muzni limeripoti kuwa mafundisho hayo ya muda ya Qur’ani yanasimamiwa na kamati ya Anwarul Qur’ani al Karim.
Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema mafundisho hayo yanatolewa kwa mnasaba wa mwezi wa Ramadhani katika msikiti wa Zainul Abidin (as) katika eneo la al Dairah kwenye mji wa Saihat.
Lengo la mafunzo hayo ni kukuza kiwango cha kiraa ya wasomaji wa eneo hilo na kutoa mafunzo ya sheria na kanuni za tajwidi.
Kamati ya Anwarul Qur’ani imesema kuwa makarii wote wa eneo la al Sharqiyyah wanaruhusiwa kushiriki katika masomo hayo. 833955