IQNA

Tarjumi mpya za Qur'ani zaarifishwa Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani, Tehran

17:35 - July 31, 2011
Habari ID: 2162806
Tarjumi mpya za Qur'ani Tukufu kwa lugha mbalimbali zimearifishwa na taarisisi ya Tarjumane Wahy katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani yanayoendelea hapa mjini Tehran.
Mbali na kuarifisha tarjumi mpya za Qur'ani kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kichina, Kiturkmani, Kikurdi, Kituruki, Kiazeri, Kinorway na Kifarsi, taasisi ya Tarjumane Wahyi pia imetoa maelezo kuhusu watarjumi, chapa, mahala tarjumi hizo zilikochapishwa na idadi ya kurasa za kila tarjumi.
Chumba cha taasisi ya Tarjumane Wahy pia kimearifisha juzuu ya kwanza ya tarjumi mpya kabisa ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa ambayo inajumuisha sura ya al Baqarah na al Fatiha na kamusi ya misamiati ya Qur'ani Tukufu. Juzuu hiyo ina kurasa 620 na imechapishwa mwaka huu wa 2011.
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yaliyoanza tarehe 26 Julai yataendelea hadi tarehe 26 mwezi ujao wa Agosti. 834048
captcha