IQNA

Jamii ya wana Qur'ani Iran kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

17:09 - August 01, 2011
Habari ID: 2163338
Wanachama wa jamii ya wanaharakati wa Qur'ani nchini Iran watakutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mwezi huu wa Agosti.
Mkutano huo utafanyika kwa munasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, amesema Mohammad Taqi Mirzajani, mtaalamu wa masuala ya mawasiliano katika Baraza Kuu la Qur'ani nchini Iran.
Amesema mkutano huo utafanyika Jumanne alasiri katika Husseinia (Ukumbi wa Kidini) ya Imam Khomeini RA mjini Tehran.
"Wataalamu wa Qur'ani, makarii, mahufadh na wanaharakati wa Qur'ani kutoka kote Iran watashiriki katika hafla hiyo", amesema.
Ameongeza kuwa qari wa Qur'ani kutoka Misri pia atasoma katika kikao hicho.
Kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, wanachama wa jamii ya wanaharakati wa Qur'ani nchini Iran hukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei.
834866
captcha