Mashindano hayo ambayo yamesimamiwa na Taasisi ya Imam Malik yamewashirikisha wasomaji 30 walioshinda katika duru za awali.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kuwahamasisha vijana na mabarobaro kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kupata wasomaji bora watakaowakilisha Guinea Conakry katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani katika nchi za Kiislamu.
Mashindano hayo yamefanyika katika vitengo vitatu vya vijana wenye umri wa zaidi ya miaka 18, vijana wa chini ya umri wa miaka 18 na vijana wenye chini ya umri wa miaka 10. 835767