IQNA

Jarida la Qur'ani la vilema wa macho lazinduliwa Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran

15:19 - August 02, 2011
Habari ID: 2164110
Mkurugenzi wa kitengo cha Chuo Kikuu cha Kidini cha Qum katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran amesema kuwa jarida la Qur'ani la malewavu wa macho (wasioona) lilizunduliwa jana katika maonyesho hayo yanayoendelea mjini Tehran.
Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Tayyib Hussaini amesema kuwa Baraza na Mawasiliano la Vyuo vya Kidini limeunda kamati inayoshirikisha vyuo vya kidini katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran. Ameongeza kuwa taasisi 132 za vyuo vya kidini zilitangaza kuwa ziko tayari kushiriki katika maonyesho hayo lakini kutokana na nafasi ndogo ni taasisi 58 tu ndizo zilizokubaliwa na zimepewa vibanda 20. Ameongeza kuwa vibanda vya taasisi hizo pia vinajumuisha vitengo vya tasnifu za taaluma ya Qur'ani, watoto na kitengo cha Haram ya Bibi Maasuma AS.
Sayyid Tayyib Hussaini amesema kuwa miongoni mwa ajenda za kitengo cha vyuo vya kidini katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran ni vikao vya kukosoa na kujadili filamu za kidini na zenye maudhui ya Qur'ani Tukufu. 835546

captcha