IQNA

Mashindano ya hifhdi ya Qur'ani ya watoto kufanyika Canada

15:39 - August 02, 2011
Habari ID: 2164126
Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani tukufu makhsusi kwa ajili ya vijana na barobaro yatafanyika tarehe 21 Agosti katika mji wa Montreal nchini Canada.
Mashindano hayo yatasimamiwa na Msikiti wa al Rawdah katika vitengo vitatu vya makundi ya vijana wenye umri wa miaka 7 hadi 12, miaka 13 hadi 16 na miaka 17 hadi 22.
Vijana wenye umri wa miaka 7 hadi 12 wanalazimika kuhifadhi sura za Waqia na al Rahman, vijana wenye umri wa miaka 13 hadi 17 sura ya Hud na vijana wenye umri wa miaka 17 hadi 22 watalazimika kuhifadhi sura ya Aal Imran.
Washindi bora watatu wa kila kundi watatunukiwa zawadi nono kutoka Kituo cha Kiislamu na Msikiti wa al Rawdah.
Pambizoni mwa mashindano hayo kutakuwepo mashindano ya kiutamaduni yaliyopewa jina la 'Mwezi Ramadhani' ambapo hadhirina wanaweza kushiriki kwa kujibu maswali yatakayotolewa msikitini hapo.
835735
captcha