Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha kimataifa katika Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO, watafiti, watarjumi na wachapishaji 23 kutoka nchi 20 duniani wanashiriki katika maonyesho ya mwaka huu. Nchi zinazoshiriki ni pamoja na Ujerumani, Indonesia, Malaysia, India na Ufilipino.
Ameongeza kuwa kitengo hicho cha kimataifa kitafunguliwa rasmi tarehe 9 wezi mtukufu wa Ramadhani katika hafla itakayohudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu pamoja na mkuu wa ICRO.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran yanafanyika katika Uwanja wa Sala wa Imam Khomeini RA hadi tarehe 25 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. 835764