IQNA

Nokia yazindua programu ya kalenda ya Ramadhani

1:41 - August 03, 2011
Habari ID: 2164236
Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu, kampuni ya Nokia moja kati ya mashirika makubwa ya utengenezaji simu za mkono duniani limetangaza programu maalumu ya ‘Kalenda ya Ramadhani’.
Kwa kila kalenda ya Ramadhani itakayoingizwa kwenye simu kupitia tovuti ya ‘NokiaFacebook UAE’ , Shirika la Nokia litatoa msaada kwa mashirika matatu ya misaada ya Imarati. Kalenda hiyo inawawezesha watumiaji kupata masuala mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhani kama vile hadithi za Kiislamu, muongozi wa Sauamu, taswira n.k.
‘Mwaka huu, kwa mara nyingine tena Nokia imeonyesha ufahamu wake wa tamaduni za kieneo na kufungamana kwake na jamii kupitia ‘Kampeni ya Ramadhani’. Tunawaunganisha watu na mwezi mtukufu na tunawahimiza kuwasaidia wanaohitajia katika jamii’, amesema Tom Farrell, Mkurugenzi wa Nokia katika eneo la chini la Ghuba ya Uajemi.
Programu zinginezo katika Kalenda ya Ramadhani ya Nokia ni pamoja na Qur’ani Tukufu, Nyakati za Sala, Hadithi, Muelekeo wa Qibla, Kalkuleta ya Zaka n.k.
835800
captcha