IQNA

Kanali za televisheni za Qur’ani na Sunna kwenye Youtube

1:28 - August 03, 2011
Habari ID: 2164305
Waziri wa Utamaduni wa Saudi Arabia ametangaza kuwa kanali za televisheni za Qur’ani Tukufu na Sunna zimeanza kurusha matangazo kwenye tovuti ya Youtube katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Taarifa iliyotolewa na Abdul Aziz Khoja imesema Wizara ya Utamaduni imechukua hatua ya kurusha matangazo ya kanali hizo kupitia Youtube ili idadi kubwa zaidi ya Waislamu waweze kunufaika.
Kanali hizo zinapatikana kwa kutumia anwani zifuatazo:
http://www.youtube.com/user/SaudiQuranTv
http://www.youtube.com/user/SaudiSunnahTv .
835719
captcha