Mashindano hayo yameandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Tabligi, na Maktaba ya Imam Khomeini RA kwa ushirikiano na Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Accra, Ghana.
Akizungumza mbele ya washiriki, Kiongozi wa Kishia katika eneo hilo Hujjatul Islam Ali Adam amewapongeza kwa mnasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani na akazungumzia umuhimu wa Qur'ani Tukufu.
Ametoa wito kwa Waislamu kuandaa vikao zaidi vya Qur'ani, tafsiri, qiraa na hifdhi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
837895