IQNA

Darul Qur'ani yaarifisha tarjumi za Qur'ani kwa lugha za kigeni

14:49 - August 07, 2011
Habari ID: 2166612
Chumba cha Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya Iran katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran kimearifisha tarjumi za Qur'ani kwa lugha mbalimbali ambazo zimechapishwa nchini Iran.
Tarjumi zilizoarifishwa ni za lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kijerumani, Kikurdi na Kituruki.
Miongoni mwa tarjumi za Qur'ani kwa lugha ya Kiingereza zilizoarifishwa katika chumba hicho ni ile ya Muhammad Hamid Shakir yenye kurasa 1310. Tarjumi hiyo ya Kiingereza pia ina tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kifarsi iliyoandikwa na marehemi Mahdi Ilahi Qamshei.
Tarjumi nyingine za Qur'ani kwa lugha ya Kiingereza zilizoarifishwa ni pamoja na tarjumi za Abdullah Yusuf Ali, Akbar Iranpanah, Sayyid Aliqoli Qarai na Maasuma Yazdan Panah.
Tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kiswahili iliyoarifishwa katika kibanda hicho imeandikwa na Ustadh Ali Juma Mayunga na imechapishwa na Taasisi ya uchapishaji ya Ansariyan ya Qum nchini Iran katika kurasa 1588. 838230



captcha